IREN UWOYA ATAMANI KUIGIZA NA NICOLAS
Muigizaji wa bongo movi ambaye pia ni mwenyekiti msaidizi wa club hiyo Iren Uwoya jana amedai kuwa anatamanani sana kufanya kazi na mwigizaji wa kimataifa toka nchini Marekani Nicolas Cage.
Msanii huyo amedai kuwa kutokana na uzoefu wa kuigiza na uzoefu alionao msanii huyo katika kuigiza tasnia ya filamu duniani ndio sababu ya kutamani kufanya kazi na msanii huyo.
Nicolous Cage amejipatia umaarufu kwenye tasnia ya filamu Marekani na duniani kote kutokana na filamu zake mbalimbali kama “National Treasure”, “Ghost Rider” ,“The Frozen Ground” na nyingine nyingi.