HAPPINESS MAGESA AINGIA KATIKA ORODHA YA WANAWAKE WENYE MVUTO
ALIYEWAHI kushikiria Taji la Miss Tanzania mwaka Happiness Millen Magesa ambaye kwa hivi sasa amejikita zaidi katika masula ya mitindo amezidi kusonga mbele na kuipeperusha vyema bendera ya nchi katika tasnia hiyo .
Mlimbwende huyo ametajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake warembo 20 barani Afrika.
Kupitia jarida la Glitz Afrika ambalo ndilo limetoa orodha hiyo ya wasichana hao Happiness ndio mtanzania pekee aliyeingia katika orodha hiyo.
Katika orodha hiyo wasichana wengi walioingia katika 20 bora wametokea nchini Ghana na Nigeria.
Kutokana na hatua hiyo Happiness ndiye msichana pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kuingia katika orodha hiyo.








