Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND ATIMIZA AHADI YAKE, ASOMESHA WATOTO WAWILI


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye anazidi kupata umaarufu Nasseb Abdul 'Diamond' awasomesha watoto wawili katika shule ya ijulikanayo 'East Africa Internation' iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Maamuzi ya kuwasomesha watoto hao imetokana na ahadi yake aliyoiweka siku ya mashindano ya watoto kucheza nyimbo yake inayojulikana kwa jina la 'Ngololo' .

Watoto hao ndio walioibuka kidedea  katika shindano hilo na kupata bahati ya kusomeshwa katika shule hiyo, ambapo Diamond alidai kuwa mshindi akipatikana hata kama anasoma shule ya kawaida atawaamisha na kuwapeleka katika shule anayoamini inatoa elimu yenye ubora.

"Siku niliyopanga kutimiza ahadi yangu ya kuwapeleka shule watoto walioshinda shindano la kucheza ngololo na kwa vile nilitaka wapate elimu bora zaidi nilikaa na uongozi wangu na kutafakari ni shule ipi itakayokidhi mahitaji ya watoto wale " alisema Diamond.

Diamond aliongozana na watoto hao ambao ni washindi  mwanzoni mwa wiki hii huku akiambatana na wazazi wao shuleni hapo kwa ajili ya kukamilisha usaili ili waungane na wanafunzi wenzao kwa ajili ya kuanza masomo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging