MUIMBAJI kutoka nchini Marekani Mariah Carey ameuanza mwaka kwa kuingiza hela zaidi ya bilioni 2 na milioni 300 kwa ajili ya kutumbuiza katika sherehe binafsi ya mtoto wa Sultan Brunei Prince Azim ambapo ameweza kuimba nyimbo zake tatu.
Sherehe hiyo ilifanyika siku ya mwaka mpya katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano Dorchester huko London nchini Uingereza.
Inasemekana kuwa katika sherehe hiyo alipata mwaliko kutoka kwa Prince Azam waliokuwa marafiki kwa miaka mingi, ambapo inadaiwa kuwa muimbaji huyo aliimba nyimbo zake tatu ikiwemo 'Always my baby'.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mail, ulidai kuwa Mariah aliambatana na mumewe pamoja na watoto wao wawili ambapo walitumia private Jet iliyowafuata Marekani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe hiyo.
Pamoja na hayo mwakilishi wa muimbaji huyo alithibitisha show ya mwanadada huyo katika herehe hiyo lakini alikataa kusema kiasi alicholipwa.
Wakati akiendelea kujibu maswali mbalimbali juu ya malipo ya muimbaji huyo, mwakilishi huyo alijikuta akitoa majibu yaliyopelekea kujulikana kile alicholipwa ingawa hakutaka kuweka wazi.








