Google PlusRSS FeedEmail

RAY C AJIANDAA KURUDI TENA KWENYE GEMU



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Rehema Chalamila, 'Ray C' amedai kulikumbuka jukwaa kwa ajili ya kufanya shoo mbalimbali ambapo ni amekaa kimya kwa kipindi cha mwaka mzima bila ya kufanya shoo yoyote kama ilivyozoeleka hapo awali.

Mwanadada huyo aliandika kupitia ukurasa wa Istagram, juu ya kukumbuka kufanya shoo mbalimbali kwa ajili ya kutumbuiza mashabiki wake ambao wanaonekana bado wanakiu naye.

"Naimiss steji vibaya mno" ameaandika Ray C katika Instagram yake hali ambayo ilizua majibu mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake ambao kila mmoja anaonesha jinsi gani wanavyomsubili.

Hivi karibuni Ray C alisikika kua ameanza kuingia studio na tayari ameshamaliza kurekord nyimbo zake zinazokamilisha albamu yake mpya ambayo bado hajaweka wazi jina la albamu hiyo.

Ray C ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye alipata umaarufu kutokana na kazi zake za kimuziki huku nyimbo mbalimbali ziliendelea kumpa umaarufu katika soko la muziki nchini.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging