Google PlusRSS FeedEmail

MILEY CYRUS AWATEMEA MAJI MASHABIKI


MSANII wa muziki kutoka nchini Marekani, Miley Cyrus ambaye haishi vituko kila kukicha ametoa kali katika tamasha lake ambapo aliwatemea maji mashabiki wake.

Msanii huyo ambaye kila anapopanda jukwaani hufanywa vituko vya aina yake huku mashabiki kubaki wakiduaa, alifanya kituko kipya alipopanda jukwaani katika tamasha ka ziara yake aliyoipa juna la Bangerz, ambapo aliwatemea maji mashabiki wake wa Tampa Florida.

Miley Cyrus alipanda jukwaani hupo akiwa amebeba chupa yenye maji, huku akiwa anaimba ndipo mizuka ilimpanda na kuwatemea maji aliyokunywa kwenye chupa aliyoibeba.


Mwimbaji huyo alikuwa anazunguka jukwaani akiwa ameshikilia chupa ya plastic yenye maji huku akizungumza na mashabiki hao waliolipa kiasi kikubwa cha pesa na bila ya wao kutarajia aliwatemea maji baada ya kupiga ‘pafu’ ili kutunza maji mengi iwezekanavyo kwenye mashavu yake.

Hata hivyo, mashabiki walionekana kukichukulia poa kitendo hicho na kuendelea kumpigia shangwe za kutosha wakati akitema maji hayo mara kadhaa kuelekea kwao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging