Google PlusRSS FeedEmail

RIHANNA AWEKA WAZI MAPENZI YAKE NA DRAKE


HATIMAYE mwanamuziki wa kike nchini Marekania Rihanna amethibitisha kutokuwa na mpango wa kurudiana tena na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Chris Brown baada ya kuweka wazi mahusiano yake mapya aliyokuwa akiyaficha kwa muda mrefu sasa.

Rihanna amethibitisha kuwa na mahusiano na mwanamuziki mwenzake Drake, ambapo wameamua kuyaweka wazi mahusiano hayo na siyo ya kificho tena mara baada ya kuwepo na tetesi nyingi juu ya mahusiano ya watu hao wawili.

Vyanzo mbalimbali vimeuambia mtandao wa TMZ, kuwa Rihanna na Drake wameamua kuweka wazi uhusiano huo kwa kuwa karibu zaidi huku mwanadada huyo kuamua kuvaa nguo za Drake.

Kama hiyo haitoshi tuu mwanadada huyo ameamua kuonesha mapenzi hayo hadaharani kwa kumfuata hadi chooni huku akiwa amevaa nguo ya mwanaume wake.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa Rihanna hutumia muda mwingi kwa kuwa na Drake kwa madai kuwa anamjali kuliko aliyekuwa mpenzi wake wa awali.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging