Google PlusRSS FeedEmail

BRAD PITT ASHAMBULIWA VIBAYA USONI NA MWANAUME ASIYEJULIKANA

Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya kumshambulia kwa makonde muigizaji maarufu duniani Brad Pitt usoni mwake katika sherehe ya ufunguzi wa filamu ya Maleficent mjini Los Angeles.

Mwandishi habari wa Ukraine Vitalii Sediuk - anayejulikana kwa kuwahahadaa watu mashuhuri duniani ,aliripotiwa kuonekana akivuka kizuizi na kumkumbatia Brad kabla ya kumpiga usoni.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa jina Vitalii Sediuk, alikamatwa na walinzi wa Brad baada ya kupambana naye na kukabidhiwa kwa polisi waliokuwa wanshika doria.

Pitt alikuwa anakutana na mashabiki wake kabla ya kushambuliwa ingawa hakujeruhiwa vibaya.Pitt na mkewe Angelina Joli ndio waigizaji nyota katika filamu hiyo mpya ya Maleficent ambayo ilikuwa inazinduliwa na kampuni ya Disney.

Msemaji wa kampuni ya Disney iliyotengeza filamu hiyo alisema kuwa walisikitishwa na kitendo hicho na kwamba polisi wanafanya uchunguzi.

Sediuk alizuiliwa na polisi Jumatano usiku akisubiri kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000. Polisi walisema kitendo cha kijana huyo kilikuwa cha maksudi ingawa uchunguzi bado utafanywa.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging