Google PlusRSS FeedEmail

D KNOB AELEZEA SIRI YA MAFANIKIO YAKE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini D Knob amejikuta akiitengeneza historia nyingine kwenye muziki wake mara baada video ya wimbo wake ‘Nishike Mkono’ kuoneshwa kupitia kituo cha Channel O ikiwa ni video yake ya kwanza kuchezwa katika kituo hicho tangu aanze Muziki, huku akidai kuwa uandishi mzuri wa Profile yake ndio sababu ya mafanikio ya wimbo huo.

Akizungumzia hatua hiyo D Knob  alisema kuwa, hatua hiyo ilikuwa kubwa sana kwake kwa kuwa tangu mwanzo alikuwa anahangaika kupeleka video zake lakini hazikuwa zinachezwa, ambapo video hiyo ilimfanya ashangae baada ya kuona inamsogeza mbali licha ya kuitoa kwa lengo la kuutambulisha tu ujio wake.

“Tangu mwanzo nilikuwa natamani nyimbo zangu zichezwe Channel O.nilikuwa najaribu process za kupeleka kule. Wananiambia ingia online jaribu kupeleka…nilipopeleka jamaa wakawa wanajibu nini, tutumie link, tutumie biography yako na nini…” Amesema D Knob.

Baada ya kupitia hatua zote alizofanya, D Knob anasema aligundua kuwa uandishi mzuri wa profile yake kuhusu safari ya muziki wake ni kitu ambacho kiliwavutia Channel O baada ya kumfahamu vizuri kimuziki kupitia profile hiyo.

“Nimekuja kushtukia profile ina matter mno..profile ya maisha yako ya muziki. Unajua wale wanaposema tutumie profile wanataka kuangali wewe umefanya nini na wewe ni nani. Profile pia ndio inaeleza everything. Sasa ile profile pia inategemea unaiandikaje.” Ameeleza D Knob.

Ameeleza kuwa kitu kikubwa kilichomsaidia katika uandishi mzuri wa profile yake ni kuwa wakati akiwa shule ilikuwa sehemu ya masomo yake.

Anasema wasanii wenzake wa karibu walikuwa wanashangaa kuona D Knob anajibiwa na Channel O na kumpa maelezo wakati wao walituma na hawajibiwi.

“Washikaji wa karibu ambao nao wanatuma video zao wakawa wanashangaa wewe mbona wanakuelekeza sana. Kwa hiyo mimi nimekuja kujifunza kwamba inabidi mtu awe na profile ambayo imeandikwa vizuri. Profile ndio everything…unajua sio kila sehemu ambayo unaweza kutia maguu na kujieleza ‘mimi ni D Knob’, lakini unaweza ukamtumia tu mtu halafu wewe ukalala halafu baadae huyo mtu akakutafuta.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging