Google PlusRSS FeedEmail

MUME WA FROLA MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI


Mfanyabiashara Emmanuel Mbasha, (32), ambaye ni mumu wa muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Frola Mbasha jana amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, kujibu shtaka la Ubakaji linalomkabili.

Mbele ya hakimu Willbaforce Rwago wa mahakama jiyo mwendesha mashtaka wa serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu eneo la Tabata Kimanga.

Alidai mshtakiwa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa)ambaye ni shemeji yake kinyume na sheria.

Mshitakiwa amekana shtaka hilo na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na wadhamini wawili ambao mmoja awe anafanya kazi katika taasisi inayotambulika kisheria au kusaini dhamana ya sh. milioni tano.

Upelelelezi wa kesi hiyo umekamilika na imepangwa kuitwa tena Juni 19 mwaka huu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging