Google PlusRSS FeedEmail

MWILI WA GEORGE TYSON KUAGWA KESHO LEADERS CLUB

Mwili wa muongozaji wa filamu na vipindi vya Television, marehemu George Tyson utaagwa kesho (June4) katika viwanja vya leaders Club, Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda kwao nchini Kenya kwa maziko.

Akizungumza na Pro-24, mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere alisema kuwa wamekuwa wakiahirisha zoezi hilo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maandalizi ya taratibu za kusafirisha mwili huo.

Ambapo ameweka wazi kuwa hivi sasa teyari wameshakamilisha taratibu mbalimbali, ingawa nyingine zinaendelea kukamilika hivi kesho shughuri za uagaji wa mwili wa mtayarishaji huyo zitafanyika katika viwanja vya Leaders Kinondoni, kisha kuusafirisha mwili huo Kenya kwa ajili ya taratibu za kuupumzisha katika nyumba yake ya milele.

“Tunashukuru Mungu mwili wa George Tyson umewasili jana Dar es salaam ukitokea mkoani Morogoro na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Kairuki, kumuaga marehemu itakuwa Leaders Club siku ya Jumanne na baada ya kuuaga mwili utasafirishwa Kenya kwa mazishi.”  alisema mwenyekiti huyo wa Bongo Movies, Steve Nyerere.

George Tyson Otieno, alifariki katika ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Gairo, Morogoro alipokuwa akitoka Dodoma na timu ya The Mboni Show kutoa msaada wa madawati kwa shule moja ya msingi na walikuwa wakirudi Dar es Salaam.

Katika gari hilo alilokuwemo marehemu Tyson, walikuwemo watu nane na yeye pekee ndiye aliyepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

 

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging