Google PlusRSS FeedEmail

MWIMBAJI AJITOA KATIKA KUNDI LA BOKO HARAM

MWIMBAJI wa kike wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23 anaefahamika kwa jina la Adokiye ameeleza anachofikiria kuhusu wasichana zaidi ya 200 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram.

Mwimbaji huyo ambaye anafahamika sana kwa comments za zinazotengeneza mijadala ambapo mara zote hizo hudai kuwa yeye ni bikira.

Mwisoni mwa wiki hii ameiambia Showtime kuwa anajitoa yeye kwa kundi la Boko Haram kama inawezekana wao kuwaachia wasichana wanaoshikiliwa na kundi hilo.

Ameamua kujitoa yeye ili iwe mbadala kwa watoto hao wa kike huku akiamini kwa kufanya hivyo wataachiwa huru.

“Sasa hivi ni saa tanto usiku, je unajua ninachofikiria? Wale wasichana wadogo, wapi walipo na nini kinawatokea muda huu. Sio sawa. Ni wadogo sana, natamani ningeweza kujitoa mimi kubadilishana nao, Wana umri kati ya miaka 12 hadi 15. Mimi ni mkubwa na nimeshazoea maisha zaidi yao. Hata kama wanaume 10 hadi kumi na mbili watanichukua kwa usiku mmoja, sijali. Nachojali waachie hao wasichana warudi kwa wazazi wao.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging