Google PlusRSS FeedEmail

TID 'AMPOROMOSHEA MATUSI' RAY C


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye pia ni mmiliki wa Top Band, TID ageuka kuwa mbogo mara baada ya kupokea ujumbe uliotoka kwa msanii mwenzie wa muziki wa kizazi kipya nchini Ray C.

TID amegeuka mbogo baada Ray C kumuomba wakutane wazungumze ambapo maombi hayo msanii huyo aliyaweka kupitia ukurasa wake wa Instagram hali iliyozusha mtafaruku kwa TID.

Mwimbaji huyo ambaye anadaiwa kuwa mmoja wa wasanii wanaotumia dawa za kulevya huenda alihisi Ray C anataka kumletea habari za kumsaidia kuachana na matumizi ya dawa hizo kupitia Methadone.

“Come let’s talk Tid ur the best musian in east Africa pls lets talk @tidmnyama.” Aliandika Ray C.

Ingawa Ray C hakufafanua katika comment yake aliyoiweka kwenye post ya picha ya TID inayotambulisha Refix ya wimbo wake ‘Asha ‘ uliofanywa na Lamar, TID aliporomosha matusi akimtaka aachana nae kabisa.

“B*tch leave me alone am not ur type also I don’t need shit from you. Ur mistake is urs nakuomba can u just f**k off, help ur boyfriend, I have never liked you, full stop.”Ameandika TID

Hata hivyo mashabiki walioandika comments zao walimshambulia tena TID kutokana na kile alichomjibu Ray C ambaye hakutaja kabisa nia ya kutaka kuzungumza na Mnyama TID.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging