Google PlusRSS FeedEmail

H-BABA YUPO TAYARI KUPAMBANISHWA



Mwimbaji H Baba ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa yeye ndiye mkali wa jukwaa aka mkali wa stage Afrika Mashariki na hakuna anaeweza kumfunika..

Akizungumza katika moja ya mahojiano yaliyofanywa kwenye kituo cha  Times Fm, H. Baba alisema  kuwa yuko tayari kupanda jukwaani kushindana na msanii yeyote ambaye anadhani ndiye mkali wa jukwaani na kwamba msanii huyo alipwe pesa yeye afanye bure kumthibishia.

“Hakuna kama H Baba kwenye stage na hakuna atakaenifikia mimi labda nife leo au kesho. Kama kuna msanii yeyote East Afrika anajua yeye ni mkali wa stage ajitokeze, mimi peke yangu na yeye peke yake. Mimi nitaperform bure yeye alipwe pesa.”

“Hata akama Tanzania kuna mtu anajijua yeye ni mkali wa stage peke yake asogee. Mimi nitaperforme peke yangu na kucheza na yeye vilevile.” H Baba ameiambia The Jump Off ya 100.5 Times Fm.

Ameongeza kuwa ameamua hivyo kwa sababu anaona kuna wasanii wanaopewa nafasi ya kuwa wakali wa jukwaa nay eye kuwekwa kando wakati hali halisi ni kwamba yeye ndiye mkali wao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging