Google PlusRSS FeedEmail

'MCHEPUKO' WASAMBARATISHA NDOA YA CIARABAADA ya mapenzi yao kuvuma Rapper Future na Ciara wameachana mara baada ya kupata mtoto mmoja mwenye miezi mitatu.

Kwa mujibu wa TMZ, wasanii hao ambao walikuwa wachumba waliovishana pete ya gharama waliachana kufuatia tabia za Future kuendekeza michepuko hali iliyompelekea Ciara kuvua pete hiyo kama mwiba uliokuwa unamchoma kidoleni.

Masaa kadhaa baada ya wawili hao kutangaza kuachana rasmi, imeelezwa kuwa mapambano mengine yameanza kuhusu mtoto na tayari Ciara ameshaanza michakato ya kisheria kumlinda juu ya malezi ya mwanae.

Ciara amepost picha ya mwanae huyo wa kiume akiwa amemuweke mkono wake hali iliyotafsiriwa kama ndicho kitu cha thamani alichobaki nacho katika penzi lao.

Future alikuwa tayari ana wanawake watatu aliozaa nao lakini Ciara aliamini mapenzi hayapimwi kwa kuangalia historia.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging