Google PlusRSS FeedEmail

OMMY DIMPOZ, NEY WA MITEGO WAPAGAWISHA SERENGETI FIESTA KAHAMA



Kwa mara ya kwanza katika historia ya burudani, Serengeti fiesta imewakuna wanakahama kwa kuwapa burudani waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu. Katika usiku huo wa burudani, zaidi ya wasanii kumi walipanda jukwaani na kuporomosha mvua ya burudani.

Kwa umahiri wasanii hao, bilakujali tofauti na aina ya muziki waliokuwa wakiimba walishirikiana katika vipengele mbalimbali wakiwa na lengo la kuwapa wanakahama burudani bora.

Ommy Dimpoz alikuwa kati ya wasanii waliokonga nyoyo za wanakahama pale alipofungua pazia la radha-pendwa, bongo flavor, kwa kuimba nyimbo zake mpya na zile za zamani. Ujasiri na umahiri wake katika jukwaa ulizidi kuongeza utamu na radha katika kipindi chote alichokuwa katika jukwaa.

Shangwe na ndirimo za mashabiki zilisikika kila pande pale mwana wa kigoma, Ommy, alipoachia vibao vyake kama vile ‘Ndagushima”, “Baadae” , “Nainai” and “Tupogo”. Msisimko ndani ya ukumbi wa Kahama stadium ulidhihirisha kwamba Serengeti Fiesta imepeleka kile walichokuwa wakikisubiri.

Wakiongea na gazeti hili, baadhi ya mashabiki walisema kwamba, “kwa burudani hii ya leo, Serengeti fiesta kiboko”.

Baada ya burudani kadhaa kutoka kwa wasanii mbalimbali, ndani na nje ya kahama, Ney wa Mitego alifunga dimba kwa kuwainua mashabiki na vibao vyake alivyokuwa akiviimba kwa umahiri mkubwa. Mirindimbo ya kibao kimoja baada ya kingine iliwafanya wanakahama wasijutie kuikaribisha Serengeti Fiesta katika mazingira yao.

Vibao kama vile “Nakula ujana”, mziki gani na vingine vingi vilisindikizwa na sauti za shangwe kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiimba pamoja nea hatua kwa hatua. Haikuwa rahisi kuwatuliza maelfu ya mashabiki zake kwani umahiri wake katika kuimba mashahiri kukiambatana na mikogo viliwafanya mashabiki washangilie kwa furaha.

“Hii ni mara ya kwanza kwa Serengeti fiesta kufika kahama, lakini inashangaza kuona maelfu ya wanakahama wakifurika uwanjani kuipokea na kuisapoti Serengeti fiesta. Ninafuraha kuona furaha katika nyuso zao, wakifurahia burudani kutioka kwa wasanii tulio waleta,” alisema Meneja wa bia ya Serengeti, Rodney Rugambo.

Bwana Rugambo aliushukuru uongozi wa serikali ya Kahama kwa kuwapa ulinzi madhubuti. “ulinzi ulikuwa imara na serengeti fiesta imeenda salama salmini,” alisema.

Aliongeza kwa kuwashukuru wanakahama kwa kuipokea Serengeti fiesta kwa mikono miwili. “ wanakahama wametuonyesha ukarimu wa hali ya juu sana. Tunawashukuru kwa kujitoa kwao na kwa kutuunga mko. Ni matumaini nyetu kwamba tutapata usherikiano kama huu tutakapokuja wakati mwingine,” alisema Bwana Rugambo.

Baada ya Kahama, burudani ya Serengeti fiesta itaelekea katika mkoa wa Tanga, Agosti 23 katika uwanja wa Mkwakwani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging