Google PlusRSS FeedEmail

YAMOTO BENDI KUFANYA MAGEUZI
KIKUNDI cha bendi ya Yamoto inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi inazidi kuendelea kufanya vizuri kila kukicha ambapo hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwemo Nibemende/Nitajuta, Niseme.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaaada mkubwa katika nyimbo zao zote.

“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada ya moja.” Amesema Asley.

“Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging