Google PlusRSS FeedEmail

AMNG'ATA MIDOMO MPENZI WAKE AKIHISI ANAMCHEPUKO

Huffington Post limeripoti habari kutoka Uingereza ya kusikitisha ya kijana Rhys Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake Chanttelle Ward mwenye umri wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na ugomvi unaohusisha na wivu wa mapenzi.

Kijana huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mpenzi wake alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akimsaliti.

Akisimulia mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza kuwa baada ya kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake msichana huyo walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo akimtuhumu kuwa anamsaliti kupitia Facebook.

Kijana huyo alichukua simu ya Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia jumbe alizokuwa anatuma Facebook lakini hakukuta mawasiliano kati ya msichana huyo na mwanaume aliyekuwa anamhisi. Moja kwa moja akaanza kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa amezifuta.

Hasira za kijana huyo zilimuogopesha akaona ni bora ampigie simu mama yake lakini alinyang’anywa simu. Rhys alifunga mlango na kuendelea kumshambulia kwa maneno Chanttelle anaeleza kuwa mgogoro huo ulipofikia hatua ya kupoa hivi, kijana huyo alimkiss huku akimuuliza kama kweli ana mpenda na hapo ndipo kila kitu kilibadilika.

“Aliweka mdomo wake wote kuzungumguka lips zangu na kuvuta, nilidhani lips zote zimetoka. Damu zilisambaa kila sehemu.” Msichana huyo alieleza.

Polisi walipofika walikuta wote wametapakaa damu usoni, wakamkamata kijana huyo na kumkimbiza Chanttelle hospitali huku akiwa na mikwaruzo katika sehemu mbalimbali za mwili.

Mwanaume huyo alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo, alieleza kuwa hakuwa na nia mbaya ya kumuumiza mrembo wake ambaye anadai alikuwa na bahati kuwa naye.

Rhys alikutwa na hatia. Alirudishwa rumande na anasubiri hukumu yake mwezi ujao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging