Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU YA CPU KUANZA KUONYESHWA TANZANIA


Filamu ya CPU ipo tayari na wakati wowote kuanzia sasa itaonyeshwa na kuuzwa nchi nzima, filamu hiyo inaingia mtaani baada ya kufanyiwa kazi na kurekodiwa katika Dvd maalum ili kulinda ubora wake kwa sababu ni sinema ya kimataifa.

Akiongea na PRO-24 msemaji wa watayarishaji wa filamu hiyo amesema kwamba sinema hiyo ilibidi itafutiwe njia rahisi ili kila mpenzi wa filamu afaidi uhondo wake kwani ni kazi ya kwanza kutengenezwa kwa Ubora na kuongozwa na muongozaji wa kimataifa..

“Ilikuwa ni lazima kujipanga katika kulinda ubora wasinema ya C.P.U ni kupata kampuni yenye sifa kwa ajili ya kurudufu kazi bora hivyo ilipelekwa Ulaya kwa ajili ya kufanyiwa kazi ili iingie katika Dvd, kwani ilikuwa ni maalum kwa ajili ya Theater,”

Filamu ya C.P.U ni sinema bora kabisa Afrika Mashariki na ilirushwa katika Jumba la sinema Mlimani City kwa siku kumi mfululizo ikijaza ukumbi na kushangiliwa na wapenzi wa filamu za kimataifa sasa inaletwa kwenu katika mfumo ulizoeleka.

C.P.U imewashirikisha wasanii nyota Tanzania kama Sauda Simba, Steven Sandhu, Nkwabi Juma, Subira Wahure, Kulwa Kikumba, Hashim Kambi, Dotnata, Mzee Korongo, Mzee Masinde na wasanii wengine wengi si ya kuikosa kaa tayari.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging