Google PlusRSS FeedEmail

MASANJA MKANDAMIZAJI AJA NA STREET PASTOR

                                    Emmanuel Mgaya
Pastor Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ amekuja na aina mpya ya uhubiri baada ya kuona pamoja na Makanisa kuwa mengi kama vile vibanda vya mitandao ya simu kwa ajili ya kutolea fedha lakini mwito bado haulidhishi, hivyo anaanzisha hudumya inayoitwa Street Gospel Ministry.

“Ninapowaambia nimeokoka watu wanaangalia nywele zangu au viatu vyangu, lakini wamesahau Samson alikuwa vipi? Sasa nakuja na Street Gospel Ministry nitahubiri mtaa kwa mtaa iwe kwa Bajaji au Bodaboda,”

“Siku hizi Makanisa ni mengi kama vibanda vya M pesa lakini watu wamekuwa wagumu kumwabudu Mungu sasa nawaletea huduma walipo mimi Mchungaji Masanja,”anasema Masanja.

Msanii huyo anadai kuwa atawafuata Kondoo walipo ili kuwachunga, na mahubiri yake atayarekodi na kutengeneza video kwa ajili ya kuwapatia wale wanaotingwa na mambo ya Kidunia ili wapate kumujua Mungu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging