Google PlusRSS FeedEmail

WEZI WA MTANDAO WAMVURUGA ADAM JUMAWezi wa njia ya mtandao maarufu kwa jina la kigeni ‘Hackers’ wameweza kuingia na kutumia akaunti ya barua pepe ya muongozaji mkongwe wa video nchini, Adam Juma.

Hackers hao wametuma barua pepe kwa kutumia akaunti hiyo wakiomba pesa kwa watu wanaowasiliana na Adam Juma.

Kupitia Instagram, muongozaji huyo wa video ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho huku wakiwatahadharisha watu kutoamini ujumbe huo.

“Daaaah kuna mtu kahack account ya email, ukiona ujumbe unaomba hela ujue sio mimi! Very sad aiseee.” Ameandika Adam Juma.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging