Google PlusRSS FeedEmail

DAKTARI ASHTAKIWA KWA KUSABABISHA KIFO CHA MUIGIZAJI MAARUFU

Melissa ambaye ni mtoto wa muigizaji na mkosoaji maarufu wa mavazi kupitia vipindi vya runinga, Joan Rivers amepanga kumfungulia mashitaka daktari aliyemtibu mama yake kabla hajapatwa na umauti.

Melissa mwenye umri wa miaka 46 amepanga kumshitaki Dr Gwen Korovin ambaye alidaiwa kutokuwa na kibali cha kufanya kazi za utabibu katika Yorkville Endoscopy Clinic huko Manhattan ambapo Joan Rivers alifariki akiwa na umri wa miaka 88.

Rafiki wa karibu wa Melissa ameiambia MailOnline kuwa Melissa yuko serious na mpango huo.

Amesema ingawa ni vigumu sana kujadili nae kitu kinachomuudhi wakati huu, lakini ataanzisha mashtaka hivi karibuni.

Taarifa zimeeleza kuwa daktari huyo licha ya kutokuwa na kibali bado anaendelea kutoa matibabu katika hospitali hiyo wakati ambapo bado anachunguzwa na vitengo vya usalama vya Marekani.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging