Google PlusRSS FeedEmail

KAULI YA CHRIS BROWN KUHUSU EBOLA YAWACHEFUA BAADHI YA WATU



Mwimbaji mashuhuri duniani ,Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.

''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu Duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown.

Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali awe kimya.

Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.

Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema.

Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.

Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging