Google PlusRSS FeedEmail

LINEX AKANUSHA UVUMI WA KUWA YEYE NI MVUTAJI BANGI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Linex akanusha uvumi unaovuma kwa baadhi ya watu na kwenye baadhi ya vyombo vya habari juu yay eye kutumia dawa za kulevya aina ya bangi, na kudai kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho tangu azaliwe.

Hali hiyo imeibuka baada ya kuwepo kwa uvumi wa muda mrefu juu ya msanii huyo kuvuta bangi kutokana na muonekano wake hali ambayo imepelekea baadhi ya waandishi kumuuliza swali hilo juu ya yeye kuvuta bangi.

Msanii huyo alitumia ukurasa wake wa facebook kujibu swali hilo ambalo lilionekana kumkera kila anapohojiwa na baadhi ya waandishi juu ya yeye kuvuta bangi ambapo aliweka wazi kuwa yeye hajawahi kuvuta bangi.

“Kwa mara ya kwanza leo nimegoma kujibu swali ambalo nimekua nikuulizwa sana na vyombo vya habari na swali lenyewe ni kuhusu mimi kujihusisha na matumizi ya uvutaji bangi leo nawajibu watanzania na wasio watanzania sijawahi kua mvutaji bangi maisha yangu yote” aliandika Linex.

Na kuongezea kuwa “ Kama nina vuta bangi mungu ananiona na kama ningekuwa mvutaji wa bangi nisingekuwa na sababu ya kukataa wavuta bangi hamuwaulizi swali hilo mimi nisiyevuta ndio kila siku nakumbana na swali hilo narudia tena sijawahi kua mvutaji bangi sina ratiba ya kutumia dawa za aina yoyote ya kulevya msinihukumu kwa muonekano wangu”.

Aliongezea na kuwaomba watu wasimuhukumu kwa muonekano wake kwani hajawahi kujihusisha na swali hilo la uvutaji bangi, ambapo si uvutaji tu pia hajawahi kutumia dawa zozote za kulevya huku akiwa anatumia muda mwingi kuutengeneza muziki wake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging