Google PlusRSS FeedEmail

MWIGIZAJI LYNDA BELLINGHAM AMEFARIKI DUNIA


Mwigizaji Mwingereza na mtangazaji Lynda Bellingham, ambaye alikuwa akiugua saratani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66, amethibitisha wakala wake.

Wakala huyo Sue Latimer amesema amefariki dunia jana "mikononi mwa mume wake.".

Mwigizaji huyo maarufu katika jukumu la muda mrefu la mama katika matangazo ya TV ya Oxo, amekuwa akiugua saratani ya utumbo  tangu alipogundulika Julai 2013.

Bellingham amesema alipanga kusitisha matibabu yake ili kuipunguzia machungu familia yake baada ya ugonjwa huo kusambaa katika mapafu na ini.

Katika taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia ya Bellingham Bi Latimer amesema: "Lynda alifariki dunia akiwa mtulivu mikononi mwa mume wake jana katika hospitali ya London.

"Familia yake ingependa kuwashukuru wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa uangalizi wao mkubwa na msaada walioutoa kwa marehemu."
Lynda Bellingham akiwa katika moja ya majukumu yake ya uigizaji katika mchezo wa "much-loved mum" katika matangazao ya Oxo 1983

Amesema: "mwigizaji, mwandishi na mtangazaji hadi mwisho ilikuwa ni taaluma ya Lynda."

Bellingham pia alifahamika kwa maonyesho kama"All Creatures Great and Small" na katika miaka ya karibuni alikuwa katika jopo la ITV la Loose Women.

Bellingham jukumu lake kubwa lilikuwa la mama aliyependwa mno katika matangazo ya Oxo kutoka mwaka 1983.

Akizungumza mapema mwezi huu, Bellingham amesema uamuzi wake wa kusitisha tiba ya mionzi ilikuwa "faraja kubwa" kwa sababu kwa kiasi fulani niliweza kujidhibiti mwenyewe".

Kifo chake kimekuja siku 10 tu baada ya kuchapishwa kwa kitabu cha kumbukumbu zake cha "There's Something I've Been Dying To Tell You".

Katika kumbukumbu hizo aliandika kuwa alikuwa anapanga kumaliza matibabu mwezi Novemba na "angependa kuona Krismasi moja zaidi, kama itawezekana"

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging