Google PlusRSS FeedEmail

NICKI MINAJ ABWAGANA NA MPENZI WAKE

Wanasema dalili ya mvua ni mawingu, hivi ndivyo inavyoonekana katika uhusiano wa Nicki Minaj na mpenzi wake Safaree Sam ambaye alikuwa amejichora tattoo yenye picha ya Nicki na jina lake pia.

Wiki hii, Safaree ameonekana akiwa kifua wazi huku akiwa ameifunika tattoo ya picha ya Nicki na jina lake kwa michoro mingine. Tattoo nyingine aliyokuwa ameichora mkononi mwake inaonekana pia ikiwa imefifia sana ikiashiria kufutwa.

Hali hii imechochea kuni tetesi zilizoanza kusambaa kuwa wamepigana chini hasa baada ya Nicki Minaj kutweet, “Single and Ready to mingle.”

Tweet ambayo kwa mujibu wa Urban Islandz haikuwa na kwa ajili ya uhusiano wake bali alikuwa anazungumzia muziki wake kuwa anayo nafasi zaidi kwa mashabiki wake wakiume.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging