Google PlusRSS FeedEmail

DULLY AELEZA SABABU YA KUACHIA WIMBO WAKE ULIOJAA MATUSI




Siku chache baada ya wimbo wake wa Thats The Way uliojaa matusi yasiyoweza kuandikika kuanza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao , msanii wa kitambo wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amefunguka kuwa halikuwa kusudio lake kuachia wimbo huo bali ulivuja kwa bahati mbaya mitandaoni.

Akipiga stori hivi karibuni, Dully alisema kuwa wimbo huo aliomshirikisha mwanadada Maunda Zorro, aliurekodi miaka nane iliyopita kwenye studio yake ya Dhahabu Records na hakupanga kuutoa lakini kwa bahati mbaya ukavuja na kuingia kwenye mitandao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging