Haijulikani kama sababu ni kuuza sana sokoni jambo ambalo halina ubishi, lakini pia inawezekana ni moja kati ya wasanii ambao gharama zao si kubwa kama alivyo msanii kama Gabo hivi ambaye kwa sasa ni gumzo katika tasnia ya filamu
Bila ubishi kweli King Majuto anauza na kufanya vizuri lakini swali la msingi linakuja hivi leo Mzee wetu akiamua kwa roho moja aseme anastaafu tasnia inasimamaje? Wale wanaomtegemea na ,kumuweka kama alama yao ya mauzo watafanya nini ili waendelee na maisha?
Maswali ni mengi tunafikiri watayarishaji hata kama ni waoga ni vema kujiandaa na kutafuta njia nyingine filamu zao ziuze hata bila kuwa na King Majuto, tuliona mfano kwa marehemu Kanumba, Sharo milionea wasanii toka waondoke hakuna msanii hata mmoja kaziba mapengo yao.
Tunahitaji kuanza kutafuta hadithi nzuri tunazipataje kwa ili mtazamaji aweze kuangalia kwa shingo upande kwa sababu hajamuona bingwa King Majuto lakini akiwaangalia na kukamatwa na hadithi awe balozi mzuri kuwaaambia wengi sinema ni nzuri.
“Ndugu yangu umri huu sihitaji tena kukimbizana na vijana location lakini sina mtaji wa kutosha mimi kwa sasa nahitaji sana Trekta niende zangu shamba nilime nimalizie maisha yangu, si kukaa mijini na umri huu wapi na wapi?,”anasema King Majuto.
King Majuto anafanya sana kazi bila kupumzika kwa sababu kila mtayarishaji anamhitaji, anaweza kurekodi sinema hadi nne kwa siku kuna wakati ambao anarekodi mchana na usiku ili amalize kazi za wateja wake ambao kila anahitaji kumtumia.
Asanteni wanatasnia tujaribu kuwa wabunifu isije ikafika wakati waigizaji wengine wakaishia kusikojulikana kwani hawataweza kushindana na soko halisi.