Google PlusRSS FeedEmail

RAY C ATABILI UJIO WAKEMwanamuziki wa siku nyingi, Ray C ametangaza kuwa atatoka mwezi huu, lakini akiwajulisha mashabiki wake kuwa safari hii ataweka nguvu zaidi kwenye uimbaji badala ya unenguaji, ambao ulimpa umaarufu.

Ray C, ambaye ametamba kurudi rasmi na kibao cha “Mshum Mshum”, amesema ingawa mashabiki wake walimzoea kwa umahiri wake katika kukata viuno, sasa watarajio vitu tofauti; muziki anaoufanya ni ule wa kuonyesha kipaji chake cha kuimba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ray C alisema mwezi huu anatarajia kurudi rasmi katika anga za muziki kwani ameshahakikisha kuwa harakati zake za kupambana na dawa za kulevya kupitia mfuko wake wa Ray C Foundation, zimesimama imara hivyo ni wakati wa kurudi ili aendelee na kampeni yake upande wa pili.

“Ninatarajia kuachia nyimbo zangu mpya za “Kiss Kiss” au “Mshum Mshum” mwezi huu, lakini mashabiki wangu wajue kwamba safari hii ni kuonyesha kipaji cha kuimba, hakuna mambo ya kiuno bila mfupa, nimebadilika kwa kiasi kikubwa sana,” alisema.

Ni kitambo toka Ray C, ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, kuonekana kwenye muziki baada ya ukimya wa muda mrefu uliotokana na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya, ambao anakiri ulimrudisha nyuma kimaisha.

“Natamani wasanii wengine wasiguse kabisa hii kitu. Binafsi imenirudisha nyuma sana. Kwa sasa nimesharekodi studio za Legendary Music Studio kwa Tudd Thomas na kwingineko,” alisema.

Ray C alizidi kufunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya pia utahusisha nyimbo za taarabu.

“Albamu yangu ambayo inakuja hivi karibuni ina mchanyiko wa nyimbo mbalimbali, zikiwemo taarab na za kihindi. Nimefanya taarab kama mbili na zook, yani nimebadilika kabisa,” alisema.

kuna kwaito, kuna bongoflava,uhindi hindi kidogo,” alisema Ray C.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging