Wasanii wamepokea kwa furaha kubwa ujio wa tuzo hizo wakisema kuwa ni mkombozi wa tasnia ya filamu kwani kuwepo kwake kutachochea ukuaji wa filamu na vipaji pia kuongezeka, Prof. Elisante alifurahia mipango ya shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).
Katibu huyo amemwahidi Rais wa Taff Simon Mwakifwamba, kuwa atahakikisha anawasaidia wasanii kuingia katika ujasiriamali ili kuwaongezea kipato na kupata uelewa katika harakati za maisha.