Google PlusRSS FeedEmail

KITIME AJITOSA BONGO MOVI

Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na karibuni amezindua sinema iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika jamii.

Katika filamu hiyo ambayo Kitime anacheza kama muigizaji mkuu, akitumia jina la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye nyumbani kwake kuna umemejua akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na baadhi ya wakazi wenzake kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani kwake.

Kwa kutumia ofisi yake, anapora ardhi za watu na mbaya zaidi anawachukia wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi anaona hawana lolote zaidi ya kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano na migogoro mikubwa ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na msisimko wa namna yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging