Akizungumza na Kituo cha Radio Times FM cha jijini Dar, wikiendi iliyopita, Jide alifunguka kuwa yeye ndiye aliyeamua kummwaga Gardner.
Katika mahojiano hayo, Jide alisema kwamba alikuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gardner lakini alisema alikuwa akiteswa
Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuzungumzia masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.
“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi siyo mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha yangu kwenye media,” alisema Jide na kuongeza:
“Ndiyo maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. “Watu wanaongea chochote wanachohisi au wanachotaka kusema. Ninavyofikiria mtu anayenipenda mimi alinijua kwa sababu ya muziki na waendelee kuliheshimu hilo kwa sababu kila mtu ana haki ya kuwa na privacy..