
“Nimefurahi sana kwa mapokezi haya hapa Uwanja wa Ndege kutoka kwa wasanii wenzangu wadau wa filamu na Familia yangu sina cha kuwalipa kwa moyo wao lakini Mungu atawalipa na kuwaongeza kilichopungua asanteni,”anasema Tico.

Baada ya kuondoka katika viwanja vya ndege vya Mwl. Nyerere aliekea moja kwa moja katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa alipata nafasi ya kuongea na wanaahabari na viongozi wa Basata kwa kushukru ushindi huo kwa kulitangaza Taifa la Tanzania.
“Tunapaswa kufanya kazi zenye ubora zinazoweza kututangaza na si bora kazi tunajivunia pale mtu anapovuka mipaka ya Taifa, tunafurahia kupokea tuzo kutoka Marekani,” anasema Agness msemaji wa Basata.