Google PlusRSS FeedEmail

JENNIFER AKANUSHA UVUMI KUWA KWA SASA ANAIMBA

            hanifa daudi
HANIFA Daudi ‘Jennifer’ msanii nyota na machachari katika tasnia ya filamu amekanusha kuhusu kuripotiwa kuwa amejiingiza katika masuala ya muziki wa kizazi kipya, bali yeye yupo katika uigizaji na si kama awali kwani anaangalia ni mtayarishaji gani anaweza kufanya kazi naye, pia yupo makini na masomo kwa sasa.

“Muda mwingi kwa sasa nautumia kwa masomo sifanyi sanaa nipo shule sijawahi kuimba wala sina wazo kama hilo sina sauti ya kuimba kuongea sana tu sauti yangu inakauka sasa iwe kuimba jamani siyo Jennefer mimi, kuigiza kwenye naangalia sinema ya kushiriki,”anasema Jennifer.


Jennifer amezidi kusema kuwa kuigiza na wasanii wengine ni changamoto tofauti na walipokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba alikuwa akiwalea kama watoto lakini watayarishaji wengine wakifanya nao kazi wanatukana hata bila kujua kama ni watoto hivyo hawezi kujiweka sana katika sanaa asiharibu masomo yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging