Google PlusRSS FeedEmail

WAKE UP YA MANAIKI SANGA YAKAMILIKA

                             Manaiki Sanga, Jack Wolper
Filamu ya Wake up au Expendables ya Bongo iliyotengenezwa na mwigizaji na mtayarishaji Manaiki Sanga ipo tayari na wakati wowote itaingia sokoni kwa ajili ya mauzo, filamu hiyo ambayo imeshirikisha wasanii nyota wenye majina  inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa Filamu.

Manaiki Sanga amesema kuwa filamu hiyo imekamilika kwa kila kitu kinachosubiriwa ni njia tu ya kuisambaza kwani angependa sinema hiyo imfikie kila mpenzi wa filamu duniani kama alivyopanga wakati wa maandalizi yaliyochukua muda na fedha nyingi.

“Nashukru mungu kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa na sasa kazi ipo tayari kama ni cha kula kinasubiriwa kuliwa tu, maana kimeshaandaliwa mezani Wake Up ni sinema ya kihistoria kwa”anasema Manaiki.

Filamu ya Wake Up imewashirikisha wasanii kama vile Jack Wolper, King Majuto, Mama Abdul, Irene Uwoya, Hemed Suleiman, Kajala Masanja, Mangi , Manaiki Sanga na wasanii wengine kibao wenye majina Swahilihood.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging