Google PlusRSS FeedEmail

GAUNI ALILOVA LUPITA NYONG'O LENYE THAMANI YA DOLA 150,000 LIMEIBIWA

Gauni lenye thamani ya dola 150,000 sawa na shilingi milioni 270 za Tanzania alilovaa muigizaji filamu wa kimataifa Lupita Nyong'o mwenye asili ya Kenya kwenye hafla ya utoaji tuzo za Oscars limeibiwa katika chumba cha hoteli huko Hollywood.

Gauni hilo lililobuniwa na Calvin Klein Collection na mbunifu Francisco Costa lina vito vyeupe vya asili, lilichukuliwa kwenye hoteli ya London Magharibi mwa Hollywood, wakati Lupita akiwa nje ya chumba chake.

Muigizaji huyo ambaye baba yake ni mwanasiasa maarufu nchini Kenya, mwaka jana alishinda tuzo ya muigizaji bora msaidizi kwa ushiriki wake kwenye filamu ya Twelve Years a Slave na siku ya jumapili alitoa tuzo ya Oscars akiwa amevalia gauni hilo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging