Picha ya Chege na Temba iliyozagaa mtandaoni yaleta chuki kati ya Chege na Miamartha, baada ya mtangazaji huyo kuweka Instagram picha hiyo iliyozungushiwa alama nyekundu kwenye mkono wa Chege ikionyesha kitambaa cheusi alichokuwa kajifunga na kuuliza kama ni Hirizi.

Kwa mujibu wa Chege, Picha hiyo ilipigwa alipokuwa akifanya show wiki iliyopita mjini Dodoma, na kitambaa hicho si hirizi, bali ni kitambaa cheusi alichofunga kuashiria kuguswa namsiba wa Mez B, kwani amefariki asubuhi wakati wao walikuwa na show mchanawa saa tisa.