Google PlusRSS FeedEmail

MOZA AFIKISHWA POLISIMoza ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo kisha kuachwa, anadaiwa kumrekodi video ya utupu Ezden kipindi walipokuwa kwenye uhusiano mzuri kisha kuisambaza mitandaoni walipogombana.

Chanzo makini kimedai kuwa, Moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar kufuatia msako mdogo uliofanywa na polisi saa chache baada ya mrembo huyo kuvujisha video hiyo.

“Wameshamtaiti pale Oysterbay, wanakamilisha tu taratibu za ushahidi kisha anaburuzwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa,” kilisema chanzo chetu, juzi Jumatano. Moza amedaiwa kuiachia video hiyo mapema wiki hii kutokana na chuki za kuona Ezden ana mwanamke mwingine hivyo akaona akivujisha video hiyo atakuwa amemkomoa mtangazaji huyo kijana aliyewahi kuwa mume wa Mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’.

Akizungumzia sakata hilo, Ezden alisema yeye ni mtu anayejiheshimu, anajitambua hivyo kitendo cha mwanamke huyo kumrekodi video hiyo hakikuwa cha kiungwana.
“Hakunitendea haki, Nimeshalifikisha suala hili polisi, taratibu za kipolisi zikikamilika anaburuzwa mahakamani,” alisema Edzen. 

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging