T.I AKANA MADAI YA WIZI
BAADA ya huku kupita kwa mtayarishaji wa muziki Pharrell na msanii Robin Thicke kulipa dola milioni 7.3 kwa familia ya Marvin Gaye sasa kibao kimemgeukia Rapa T.I. kwa madai kuwa inasemekana na yeye ni miongoni wa wasanii wanaoiba mawazo ya watu.
Hali hiyo imeibuka mara baada ya kulipwa dola milioni $7.3 kutoka kwa producer Pharrell na msanii Robin Thicke, Familia ya Marvin Gaye sasa imeanza kumhughulikia rapa T.I ambaye pia ameweka sauti kwenye wimbo wa “Blurred Lines”.
T.I Ameulizwa na Tmz kuhusu kesi hii nakujibu ” Sijui kinachoendelea, sihusiki na hio kesi kabisa na mimi napenda sana kazi za Marvin Gaye, ila nawakubali sana Pharrell na Robin, Mimi ni mwandishi, mbunifu, siibi mawazo ya watu, na mtu yeyote mwenye akili ataona hilo”.








