Google PlusRSS FeedEmail

RIHANNA AGEUKA KUWA MPAMBE


Mwanadada Rihanna haishi matukio mara baada ya siku ya jumatatu kuamua kuwa mpambe wa rafiki na mfanyakazi wake anaemsaidia kuimba jukwaani Jennifer Morales aliefunga ndoa na mpenzi wake Aaron Davis huko Hawaii.

Harusi hiyo iliyofanyika huko hawai Rihanna alionekana mwenye furaha na alipendeza kwa vazi jeupe la harusi aliliovaa huku wengi wakimsifu kwa kitendo hicho alichokifanya.

Rihanna alisema aliamua kuonyesha upendo kwa mfanyakazi wake huyo ambapo habari zinaeleza kuwa ni rafiki yake kipenzi wa siku nyingi kama ishara ya upendo na shukrani kwa shughuli zao za mziki wazifanyazo kila kila siku.

Kwenye mtandao wake wa instagram rihhana alipost picha za harusi na kuandika ujumbe, “Hatiamaye ni rasmi sasa Jennifer Morales na Aaron Davis ni Mr na Mrs, nimefurahia jambo hilo”.

Je kitendo hicho kitamshawishi rihhana nae kutaka kuolewa?, Ngoja tuone nini kitatokea.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging