Google PlusRSS FeedEmail

BIRDMAN ALIHUSIKA KUPANGA MASHAMBULIZI YA KUMUUA LIL WAYNE

Jimmy Winfrey meneja wa zamani wa rapper Young Thug, na mshitakiwa namba moja anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia Lil Wayne na msafara wake mwezi April, amesema Bosi wa Cash Money Birdman nae alihusika katika upangaji wa tukio hilo.

Mtandao wa TMZ ambao umedai kuona nyaraka za maelezo aliyoyatoa Jimmy, yakieleza kuwa mlengwa mwingine wa mashambulizi hayo alikuwa ni muhasibu wa kampuni ya Cash money.

Taarifa na ‘data’ za simu zinaonesha kwamba, masaa mawili kabla ya shambulio kutokea mshitakiwa aliwasiliana na namba inayoaminika kuwa ni ya Rapper Birdman.

Birdman na mwanae Lil wayne, wametajwa kuwa kwenye ‘battle’ nzito ya kudaiana dolla za kimarekani $51 million.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging