Google PlusRSS FeedEmail

HABARI NJEMA KUTOKA NIGERIA

                  
Muimbaji mrembo wa nchini Nigeria, Seyi Shay, amedai kuwa kupitia utafiti aliofanya, amegundua kuwa Tanzania ina wasanii wakali Seyi Shay anayefanya vizuri sasa na wimbo wake, Right Now

“Nimekuwa nikifanya utafiti wangu,  [Tanzania] mna wasanii bora Afrika, sidanganyi kabisa,” alisema. “Nasubiri sana siku moja wote tuweze kukutana na kufanya wimbo mmoja mkubwa wa wasanii wa Afrika,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Seyi alidai kuwa amemfollow Alikiba lakini yeye ameshindwa kumfollow na amemuomba afanye hivyo. Seyi Shay ni miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa mwaka huu kutoa album na hivi karibuni ..Staa huyu amethibitisha kuwa Albamu  yake inatoka November 2015.

Seyi Shay amesema album itaitwa “Seyi or Shay” na itatoka Ijumaa ya November 13, 2015. Kutakuwa na pati ya kusikiliza album na nyimbo zake kama ‘Irawo’, ‘Right Now’.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging