Google PlusRSS FeedEmail

WOLPER AMRUDIA MUNGU

MSANII wa filamu nchini Jacqueline Wolper, amewataka wasanii wenzake kumrudia mungu na kufanya yale yaliyomema katika jamii, ambapo yeye amedai kuwa baada ya kufanya mengi ya kumchukuza mungu sasa ameamua kumrudia mungu wake.

Wolper alisema baada ya kufanya mambo mengi maovu ameamua kumrudia Mungu,hata kwa kusoma vitabu vyake vitakatifu kwani baadhi ya mastaa wamekuwa na kasumba ya kumsahau Mungu na kufuata ya Dunia.

Wolper alisema mara nyingi mastaa hujisahau kwa kuendekeza anasa nyingi za duniani na kumkosea Mungu na ni bora kutenga muda hara kwa saa mbili kwa siku kusoma neno la Mungu.

Aliongeza baada ya kutambua hilo,ameamua kubadilisha mfumo wa maisha yake na kutoruhusu kutawaliwa na mambo ya kiulimwengu na kumrudia Mungu wakiwa na shida.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging