Google PlusRSS FeedEmail

20% AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUPATA TUNZO 5

Baada ya kushinda tuzo 5 za Kili Music Awards 2010/2011 na kuweka historia,Alwatan 20% amefunguka kuwa hakutegemea kama angeshinda tuzo zote 5 kwenye vipengele ambayo ameshiriki!
"Sikutegemea kama ningepata tuzo hizo zote 5 kwani nilitegemea tuzo 2 kiuhakika....ya wimbo Bora wa Afro Pop na Mtunzi Bora wa Nyimbo,ila kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume,Muimbaji Bora wa Kiume na Wimbo Bora wa Mwaka - Tamaa Mbaya,kiukweli sikutegemea kabisa"

Kuhusu Producer wake Man Water wa Combination Sound  kutopata tuzo ya Mtayarishaji/Producer Bora wa Muziki-2010,20% amesema kuwa Man Water alistahili kama yeye amepata tuzo zote 5 kupitia nyimbo ambazo Man Water amezitengeneza za Malumbano na Tamaa Mbaya,lakini tuzo imeenda kwa Producer Lamar toka FishCrab Studio haiko sawa kabisa...alifunguka 20% akiwa njiani kurejea Dar 

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging