Nyota wa filamu Tanzania Aunty Ezekiel yupo location akirekodi filamu mpya inayojulikana kwa jina la Same Girl, filamu hii inatayarishwa na kampuni ya Mapunda Entertainment Limited ya jijini Dar es Salaam, filamu hii ilianza kurekodiwa toka wiki iliyopita na ipo katika hatua za mwisho kabisa ikimaliziwa scene chache zilizobaki na kisha kuingia katika uhariri.
Katika filamu hii Aunty Ezekiel anacheza akiwa mhusika mkuu wa filamu hii, katika filamu hii ambayo inajaribu kuelezea jinsi gani mapenzi yanavyoweza kuwachanganya ndugu, rafiki na jamii nzima kwa ujumla na kujikuta badala ya kuishi katika amani wanageuka na kuwa maadui na kuvunja uhusiano kwa sababu ya mapenzi, akiongelea filamu hiyo mtunzi na muongozaji wa filamu hiyo Selles Mapunda amesema kuwa.
“Same Girl ni kitu tofauti sana japo inaongelea masuala ya mapenzi lakini kwa njia nyingine ya maisha na wasanii ambao wapo katika filamu hii, wameonyesha uwezo wa ziada sana kama vile walikuwa katika mashindano, hivi sasa tupo katika hatua za mwisho kabisa katika kumalizia filamu hii toka tulipoanza tumenda vizuri, jambo la kusubiri ni uhariri tu” Alisema Selles Mapunda.
Katika Same Girl kuna nyota wengine walioshiriki katika filamu hii kama Benny Kinyaiya, Steve Sandhu Aunty Ezekiel mwenyewe ambaye ni Steringi, huku ikiongozwa na Director Selles Mapunda ikiwa imetungwa yeye mwenye Producer wa filamu hii ni Steps Entertainment.