Google PlusRSS FeedEmail

CHRISS MHENGA ASEMA FANI YA FILAMU NA MAAIGIZO IMEVAMIWA NA WAUZA SURA

Muasisi wa kundi la Kaole Sanaa Group ambalo limeonekana kuwa ni chanzo cha wasanii wengi nyota katika tasnia hii, Chrissant Mhenga amesema kuwa hali ya sasa si nzuri katika tasnia ya filamu na maigizo kwa ujumla katika kuzalisha wasanii wapya zaidi ya wauza sura tu, Chriss ambaye ni mtayarishaji, muongozaji na mtunzi wa filamu na maigizo nchini ameendelea kuelezea kuwa zamani wasanii sanaa ilikuwa katika damu.
Chriss aliongea hayo baada ya kufanya mahojiano na waandishi wa habari kuhusu hali ya kushuka kwa kiwango katika makundi mengi ambayo yanaendelea kuigiza katika Televisheni, hivi sasa makundi mengi yameshindwa kabisa kuonyesha uwezo wa uigizaji tofauti na siku za nyuma wakati ilikuwa kila mtu inapofika siku za michezo hii kuruka katika Televisheni watu wote walikuwa karibu kabisa na Runinga zao kwa ajili ya kuangalia mchezo husika.
“Wakati mimi nikiwa naongoza kundi hili la Kaole wasanii wengi waliokuja kujiunga na kundi hili walikuwa na nia moja tu kuja kufanya kazi lakini si kwa sasa watu wanajiunga na makundi ili waonekane katika runinga na kufanya mambo yao tu, wakati Kaole ipo juu na kupendwa na kila mtu hakukuwa na fedha kabisa lakini wasanii kwa sababu usanii ulikuwa katika damu bado waliigiza katika kiwango kikubwa, lakini leo hii fedha zipo na hakuna lolote” Anasema Chriss.
Aidha ametoa mfano kuwa wale wasanii ambao kwa wakati ule walijitoa ndiyo leo wapo juu na wamefanikiwa katika tasnia hii anasema kwa mfano msanii kama Vincent Kigosi (Ray), wakiwa location alikuwa lazima ashike (Boom mic) kipaza sauti mara kabeba stand, alifanya kazi kwa moyo wasanii ndani ya kundi kulikuwa na mashindano wasanii kwa wasanii katika kuigiza kitu ambacho anaamini kuwa kilisaidia sana uwezo wa wasanii kukua zaidi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging