FM ACADEMIA WAFUATA NYAYO ZA TID WAJITOA KATIKA TUNZO ZA KMA
Posted on by Unknown
Mara baada ya mwanamuziki wa kizazi kipya Tid kusema na kutota kushirikishwa katika Tunzo kubwa za muziki Tanzania KMA Hatimae wanamuziki wa Bendi Fm Academia kupitia Rais wake Nyoshi El Saadat wamedai kuwa hawataki kushiriki katika tuzo za Kilimanjaro Music Award 2011,kutokana na kutotendewa haki.Nyoshi amesema kuwa kamwe hawautambui umuhimu wa Tunzo hizo na wao kama bendi ya dansi ndio maana wameamua kujitoa na hawataki kushiriki tunzo hizo,kwa mujibu wa Nyoshi alisema “hawa kili bwana wanacheza na akili zetu na shangaa kwanini kipindi hiki Album yetu ya Vuta Nikuvute haikupata nafasi ya kushirikishwa katika kinyanganyiro cha Albamu bora ya mwaka ya bendi , au ni kwasababu bendi walizokuwa wanazitegemea kutoa Album hawakutoa mwaka jana? Aliendelea kusema Tulitoa Albam lakini kwanini wanatuonea sikuzote alihoji”