Wasanii 13 wa kundi la Five Star Modern Taarab wamefariki duniani mkoani Morogoro kwa ajali ya gari. Ajali hiyo ilitokea saa 2:30 usiku wa jana huko Mikumi wakiwa njiani wakitokea Kyela mkoani Mbeya, baada ya Coaster waliyokua wanasafiria kuligonga lori lililokua limepaki barabarani,na mmoja wa waliofariki ni pamoja na kinara wa kundi hilo Issa Kijoti,Sheba Juma,Nassoro Madenge,Husna Mapande,Omary hashimu na Mwanamuziki Mkongwe wa Taarab nchini,Bi Mwanahawa Ally amejeruhiwa kwenye ajali hiyo,ambaye alikwenda kulipa tafu kundi hilo.Huku majeruhi wengine wakipelekwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogogo.
Kibaya na cha kusikitisha ni kuwa wakati ajali hiyo imetokea,raia wengine walikua wanachukua kila walichokiona mbele yao,zikiwemo spika na vitu vingine vya majeruhi huku ikiripotiwa kuwa hali ni ngumu kutambua maiti
Na polisi mkoani Morogoro wanafanya kila linalowezekana zitambulike! POLE FIVE STARS MODERN TAARAB,NA WAPENZI WOTE WA TAARABU HAPA NCHINI,,









