Serikali kupitia wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo (idara ya utamaduni) imefunguka kuwa studio ya kurekodia muziki (mastering studio) iliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni ya wasanii waliyoiomba na hao ndiyo waliokabidhiwa.
Msimamo huo wa serikali umekuja baada ya kuwepo utata toka kwa wadau wa muziki wa kizazi kipya kuhusu,hasa chama cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) na Kampuni ya Fleva Unit kuwa nani hasa aliyekabidhiwa studio hiyo,na kudaiwa kuwa studio hiyo ya Rais Kikwete imetolewa kufuatia maombi zaidi ya kumi na moja yaliyotolewa na wasanii waliohudhuria sherehe za miaka mitatu toka kuanzishwa Nyumba ya vipaji nchini (THT) na imekabidhiwa kwa wasanii hao waliokuwepo kupitia Kampuni ya Fleva Unit ambayo imesajiliwa kwa msajili wa makampuni nchini (Brela) wiki moja iliyopita