Wadau wa Sanaa wameiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwawezesha maafisa utamaduni ili kusukuma shughuli za sanaa na utamaduni katika ngazi za wilaya na mikoa. Wakizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),wadau hao walisema kwamba,maafisa utamaduni wamekuwa wakipewa bajeti ndogo kiasi cha kufanya shughuli za sanaa na utamaduni kushindwa kuendelea na kukwama kabisa. Sekta ya sanaa imekuwa ikishughulikiwa na wizara tatu tofauti akimaanisha ya Viwanda na Masoko,TAMISEMI na ile ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo hali ambayo imekuwa ikisababisha migongano ya kiutendaji na ukosefu wa usimamizi wa moja kwa moja wa sekta hii katika wizara moja.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.